UJUMBE WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA -MBEYA WATEMBELEA BMH KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA KUBORESHA HUDUMA KWA WAGONJWA
Na. Jeremiah Mbwambo,
Picha: Jeremia Mwakyoma
Dodoma Agosti 24, 2026
Viongozi wa Hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini-Mbeya wamefika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ili kujadili kwa pamoja maeneo ya kuboresha huduma wanazozitoa kwa wagonjwa
Akiongea mkuu wa msafara Dkt. Raphael Gabriel amesema tukiungana kubadilishana uzoefu tutawahudumia wananchi kwa kuwajali
"Leo tumekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, wametutembeza katika maeneo ya kutolea huduma hakika huduma za BMH ni zakipekee sana katika kumjali mgonjwa wanapomuhudumia"Amesema Dkt. Raphael
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Abdallah Baja amesema ujio wa viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya nyanda za juu kusini unaleta taswira chanya ya namna tunavyo shirikiana katika kuwahudumia wagonjwa
"Viongozi na wataalamu wanapofika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kujenga uwezo wa namna ya kutoa huduma hii inatungengea uwezo wote kwa kuwa nao wakiwepo hapa wanatueleza mapungufu yetu nasi tunayaboresha nao wanaondoka na mazuri yaliyopo BMH"Amesema Dkt. Baja
Hospitali ya Benjamin Mkapa imetimiza miaka kumi ya kutoa huduma huku ikiimarisha zaidi huduma kwa mgonjwa kuanzia anapopokelewa mpaka anapo ondoka.