WABUNGE WAITIKIA KUPIMA AFYA KATIKA KAMBI YA KIBINGWA WAKATI WA BAJETI YA AFYA , BMH YANUFAISHA 174.

Published: May 14, 2026
WABUNGE WAITIKIA KUPIMA AFYA KATIKA KAMBI YA KIBINGWA WAKATI WA BAJETI YA AFYA , BMH YANUFAISHA 174. cover image

Na Jeremia Mwakyoma
BUNGENI DODOMA - MEI 12, 2026

Kambi ya huduma za kibingwa bobezi iliyokuwa imeandaliwa na Wizara ya Afya ikijumuisha Hospitali za Taifa na Kanda kwenye viwanja vya Bunge imehitimishwa leo ambapo jumla ya wadau 174 wamenufaika na huduma katika Banda la Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Akizungumza mara baada ya kukagua utoaji wa huduma kwenye kambi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amepongeza taasisi zilizoshiriki kwa kutoa huduma bora kwa Wahe. Wabunge na Wadau wengine bungeni hapo na kusisitiza ushirikiano baina ya Taasisi hizo katika kuwahudumia wananchi.

"Wote tunamuhudumia mteja mmoja, Hospitali zote na taasisi za Afya tunapaswa kusaidiana ili kuhakikisha mwananchi anapata huduma bora, taasisi moja ikiwa na changamoto ni jukumu la taasisi zingine kusaidia ili kuhakikisha tunafanikisha kuwapa wananchi huduma bora za Afya" alisisitiza Dkt. Shekalaghe.

Nae Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesisitiza BMH kuendelea kuweka mkazo kwenye eneo la Huduma kwa mteja(customer care).
Wahe. Wabunge wameonesha kufurahishwa kwa kusogezewa huduma karibu ambapo katika kambi hiyo ya siku mbili, BMH ilipeleka huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo, macho, mifupa, masikio pua na koo, huduma ya tiba lishe na chakula na elimu kinga ya magonjwa.