NBC MARATHON MWAKA HUU YAITENGEA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA MILION 200
Na. Jeremiah Mbwambo, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi ameeleza sababu ya kutenga milioni 200 maalumu kwa ajili ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.
" Serikali imefanya mambo makubwa sana katika hospitali ya Benjamin Mkapa, nasi tumeona tunakila sababu hizi mbio kutoa shilingi milioni 200 kusaidia mfuko wa matibabu" amesema Sabi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi ameeleza ukubwa wa ugonjwa wa selimundu kwa Tanzania
"Zaidi ya watoto elfu 14 huzaliwa na vinasaba vya sickle cell kila mwaka hivyo hufanya Tanzania kuwa ya tatu africa na ya nne Duniani kwa kuwa na wagonjwa hawa, ugonjwa huu ni gharama kuutibu huu ugonjwa kwa mtoto mmoja ni milioni 75" amesema Prof. Makubi
Ameongeza kuwa ushirikiano huu wa NBC kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa unatafsiri mambo manne
"Kwa kujitoa huku kunaonesha moja ni mbio zinazo kusudia kuokoa uhai wa watanzania, pili imeonesha NBC haipo peke yake kibiashara pekee, tatu inatoa tafsiri NBC inaweza kushirikiana na taasisi nyingine na mwisho pesa hizi zitasaidia kupanua zaidi huduma ya upandikizaji uloto" amesema Prof. Makubi
Hospitali ya Benjamin Mkapa inaadhimisha miaka 10 za utoaji huduma, huku ikiwa imeanzisha mfuko maalu wa matibabu ya figo na SelimunduΒ