WATUMISHI WAPYA WA BMH WAPATIWA MAFUNZO YA HUDUMA KWA MTEJA NA MAADILI YA UTUMISHI

Published: Feb 24, 2026
WATUMISHI WAPYA WA BMH WAPATIWA MAFUNZO YA HUDUMA KWA MTEJA NA MAADILI YA UTUMISHI cover image

Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Mkubi amefungua mafunzo kwa watumishi wapya na walio hamia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa

Amewasisitiza watumishi kufuata utamaduni wa familia ya Hospitali ya Benjamin Mkapa ambao ni.

1. Kuvaa viatu vya mgonjwa kwa kutoa huduma bora
2. Kuwajibika ipasavyo kwa wagonjwa
3. Kuwa na huduma bora kwa wateja
4. kuwa na sense of Ownership na uzalendo kwa Hospitali
5. kuboresha mawasilianao na mrejesho
6. kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja
7. kuheshimiana
8. kutanguliza kwanza huduma ya mgonjwa
9. kujiongeza na kuwa wabunifu katika kutatua kero za wagonjwa na Hospitali
10. kuwa watu chanya wa kukubali kubadili mitazamo yetu

"Mmeingia kwenye familia inamaono (Vision) ya kutibu kwa kutumia vifaa vya kisasa na ni hospitali ya kufundishia, hivyo hospitali ya Benjamin Mkapa inafanya kazi kwa ukaribu na chuo kikuu cha Dodoma" amesema Prof. Makubi

Ameongeza kuwa mmekuja kuwajibika kwa kuwatumikia wananchi wanaofika hospitali

"Mmekuja eneo ambalo siyo la kupumzika, hapa ni zaidi ya hospitali binafsi kwa kuwa uwajibikaji kwa kutoa huduma kwa wagonjwa ni wakiwango cha juu hivyo ninyi mmekuja kuongeza kasi ya uwajibikaji" amesema Prof.  Makubi

Hospitali ya Benjamin Mkapa inautaratibu wakuwapatia mafunzo watumishi wapya ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa