Mwanzo / Huduma Zetu / ZAIDI YA WATOTO 1000 WAPATIWA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU KWENYE KAMBI YA KUMUENZI DKT. GEORGE DILUNGA

ZAIDI YA WATOTO 1000 WAPATIWA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU KWENYE KAMBI YA KUMUENZI DKT. GEORGE DILUNGA

Published on June 05, 2025

Article cover image

Na Gladys Lukindo na  Carine Senguji Juni 4, 2025, DODOMA.

Zaidi ya watoto 1000 wamepata huduma za matibabu na uchunguzi katika kambi ya kumuenzi aliyekua Daktari katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. George Dilunga ambapo kambi hii imeendeshwa na madaktari Bingwa kutoka hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na ABBOTT FUND Tanzania.

Akizungumza katika kambi hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura, Dkt. Winnie Msangi amesema kuwa mpaka sasa takribani watoto 1000 wamepata huduma za uchunguzi wa awali na wengi wao wana tatizo la masikio na macho na walionekana wanahitaji matibabu zaidi wamepewa rufaa kwenda Hospital ya Benjamin Mkapa kwa uangalizi zaidi.ZAIDI YA WATOTO 1000 WAPATIWA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU KWENYE KAMBI YA KUMUENZI DKT. GEORGE DILUNGA

Na Gladys Lukindo na  Carine Senguji Juni 4, 2025, DODOMA.

Zaidi ya watoto 1000 wamepata huduma za matibabu na uchunguzi katika kambi ya kumuenzi aliyekua Daktari katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. George Dilunga ambapo kambi hii imeendeshwa na madaktari Bingwa kutoka hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na ABBOTT FUND Tanzania.

Akizungumza katika kambi hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura, Dkt. Winnie Msangi amesema kuwa mpaka sasa takribani watoto 1000 wamepata huduma za uchunguzi wa awali na wengi wao wana tatizo la masikio na macho na walionekana wanahitaji matibabu zaidi wamepewa rufaa kwenda Hospital ya Benjamin Mkapa kwa uangalizi zaidi."Tumefanya Kambi hii ya uchunguzi na matibabu katika Shule ya Msingi Dodoma Makulu kwa ajili ya kumuenzi Dkt. George Dilunga kwani alikua anakuja pamoja na madaktari wengine wa BMH kutoa huduma , na katika kambi hii tumebaini asilimia 50 ya watoto wana tatizo la masikio na macho na wamepata matibabu na baadhi ya wazazi wameshauriwa kufikisha watoto wao BMH kwa matibabu zaidi," amesema Dkt. Winnie

Dkt. Winnie amebainisha ugonjwa mwingine ambao waliona unasumbua watoto shuleni ni pamoja na matatizo ya mzio (allergy) pamoja na shida ya ngozi.

"Wanafunzi wengi wana matatizo ya ngozi yani vipele vidogo vidogo na fangasi ya ngozi na wengine mzio (alegy) katika ngozi ," ameongeza Dkt. Winnie.

Dkt. Winnie Msangi ameshukuru ABBOTT FUND Tanzania kwa kuwezesha kambi ya kumuenzi Dkt. George kufanya uchunguzi na matibabu kwa wanafunzi kwa mafanikio makubwa.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Dodoma Makulu, Mwl. Joyce Steven, ameshukuru madaktari wa BMH kuleta kambi ya matibabu shuleni hapo kwani imekuja kwa muda sahihi na huduma nzuri zimetolewa na wameomba kambi iwe endelevu hata ifanyike mara moja kwa mwaka.
“Tunashukuru kwa kutusogezea huduma hii karibu kwani imesaidia watoto ambao hawana uwezo kupata huduma nyingi kwa wakati moja na tunaomba zoezi hili liwe endelevu”, amesema Mwl. Joyce.

Mwanafunzi katika shule ya Dodoma Makulu, Mwanaidi Hassan ameshukuru madaktari kwa huduma nzuri za matibabu alizopata.

"Nawashukuru sana madaktari wa BMH kwa kutusogezea huduma karibu , nilikuwa na tatizo la sikio nimepata matibabu na naendelea vizuri kabisa”, amesema Mwanaidi.

Mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya Msingi Makulu , Juma Mohamed , amefurahishwa na kuona madaktari wengi wamekuja kutoa huduma shuleni na ameomba zoezi hili liwe endelevu kwani ili wanafunzi endelevu ili wanafunzi ambao hawana uwezo waweze kupata matibabu