WAGONJWA WENYE MAWE KWENYE MFUMO WA MKOJO WAKITOLEWA MAWE KWENYE FIGO SASA KUKAA WODINI MASAA 24 BADALA YA SIKU 5

Published: Oct 23, 2025
WAGONJWA WENYE MAWE KWENYE MFUMO WA MKOJO WAKITOLEWA MAWE KWENYE FIGO SASA KUKAA WODINI MASAA 24 BADALA YA SIKU 5 cover image
Na. Jeremiah Mbwambo
Picha na Jeremiah Mbwambo 
Dodoma  Okt. 23, 2025
 
Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa mfumo wa mkojo Okoa Sukunala wakati wakiendelea na matibabu ya kuondoa mawe kwenye mfumo wa mkojo katika kambi maalumu inayo endeshwa na madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya ACIBADEM ya nchini Uturuki 
 
"Hospitali ya Benjamin Mkapa inavifaa vya kisasa vinavyo wezesha kufanya matibabu ya kutoa mawe kwenye mfumo wa mkojo bila kufungua mwili ni kwakutumia matundu madogo (laparoscopic)" amesema Dkt. Okoa
 
Ameongeza kuwa kunafaida nyingi za kutumia teknolojia hii ya matibabu 
 
"faida ni nyingi lakini nieleze moja kubwa ambayo inamuondolea adha mgonjwa akishafanyiwa matibabu haya atakaa wodini kwa muda usiozidi masaa 24, ambapo awali ilikuwa inamlazimu kukaa wodini siku tano" amesema Dkt. Okoa 
 
Hospitali ya Benjamin Mkapa inaadhimisha miaka kumi ya utoaji huduma huku ikiendelea kuboresha huduma zake huku ikijikita katika matibabu ya teknolojia ya hali ya juu