PROF. MAKUBI ATETA NA MADAKTARI BINGWA WA JUU WA BMH NA UDOM
Published on April 28, 2025

Na Jeremiah Mbwambo, 28/04/2025 Dodoma
PROF. ABEL MAKUBI MKURUGENZI MTENDAJI AZUNGUMZIA.
1. HUDUMA ZA HOSPITALI
2. MAPATO YA HOSPITALI
3. UWAJIBIKAJI NA MAADILI YA MADAKTARI BINGWA
Tulikutana hapa mwaka jana natukakubaliana baadhi ya mambo ambayo tumeendelea kuyaboresha na kuleta matokeo mazuri kwa Taasisi yetu na kwa wagonjwa.
"Kwa kweli katika kuendelea kuboresha huduma niwapongeze tumeendelea kufanya vizuri zaidi hadi tumetambuliwa na Wizara ya Afya kama Hospitali bora ya kanda inayotoa huduma bora kwa Wananchi, hongereni sana , alisema Prof. Makubi
Ameongeza kuwa uwajibikaji na maadili kwa madaktari Bingwa ni kiapo chetu katika kuwahudumia wagonjwa, hatupaswi hata kuhisiwa vibaya juu ya mwenendo wetu
"Katika matibabu wapo wenzetu wachache wanao weka dosari na wakati mwingine tukahisiwa vibaya kwababu ya kutokuwa makini, kwa mfano Daktari Bingwa anaweka list kubwa ya kuwahudumia wagonjwa halafu baadae anawaacha wengine au anasema muda umeisha na kuahirisha huduma hii inaleta hisia mbaya kwa wagonjwa, wote mnafahamu huwezi kumuacha mgonjwa wakati amefika kwako hivyo ninawataka wote kukumbuka wajibu wetu na kiapo chetu mgonjwa akifika kwako na ukamuweka kwenye list basi muhudumie" alisema Prof. Makubi
Prof Makubi amewaomba madaktari huo kujitoa zaidi kwa ajili ya huduma bora kwa Wananchi , kuongeza ubunifu wa huduma za kisasa na kuwasimamia wenzao pamoja na Wanafunzi.
Kwa upande wake CPA. Ambele Msika Mkurugenzi wa Mipango na Fedha ameeleza kila mtumishi anatakiwa kuisaidia Hospitali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
"Nimuhimu wote kwa umoja wetu kutunza vifaa vya matibabu ili vidumu,pia kuzima taa muda usio hitajika na kufunga maji ili kuondoa bili kubwa" alisema CPA. Mssika.