KAMSHNA TUME YA UTUMISHI WA UMMA AIPONGEZA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KWA KUTOA HUDUMA BORA
Na. Jeremiah Mbwambo, Dodoma, 20/11/2025
Kamishna tume ya utumishi wa umma Bw. Hassan Kitenge ameyasema hayo alipokuwa akifungua Kikao cha Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma
"Tunafungua Kikao cha Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma, niseme Hospitali ya Benjamin Mkapa mnasifika kwa huduma bora na hii inadhihirisha mnafanya kazi kubwa hivyo ukaguzi huu utawezesha kuanzia hapa mlipo kwenda mbele, nami ninawaombea muwe Hospitali bora Africa" amesema ย Kamishna Kitengeย
Akimkaribisha Kamishna, Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Makubi amesema yupo tayari kwa Kikao cha Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma
"Kamishna nikuhakikishie tutawapatia ushirikiano wakila kitu mtakacho hitaji katika Kikao cha Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma" amesema Prof. Makubi