KAMBI YA MADAKTARI BINGWA BOBEZI WA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA WILAYANI MASASI YAHITIMISHWA RASMI, WANANCHI ZAIDI YA 700 WANUFAIKA, UPASUAJI ZAIDI YA 60

Published: Jul 04, 2026
KAMBI YA MADAKTARI BINGWA BOBEZI WA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA WILAYANI MASASI YAHITIMISHWA RASMI, WANANCHI ZAIDI YA 700 WANUFAIKA, UPASUAJI ZAIDI YA 60 cover image

Na Jeremia Mwakyoma
MASASI MTWARA - JUNI 5, 2026


Mratibu wa Kambi hiyo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Emiliana Myovela amesema kuwa zaidi ya Wananchi 700 wamehudumiwa kwenye kambi hiyo huku Wananchi zaidi ya 60 wamepatiwa huduma za upasuaji.

"Idadi kubwa ya upasuaji ilihusisha magonjwa ya macho, mfumo wa mkojo na via vya uzazi kwa wanaume ikijumuisha Tezi Dume, Ngiri maji, Ngiri Kavu na magonjwa mengine; Aidha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama Presha imeonekana kuwapata wananchi wengi pasipo wao kujua jambo linaloweza kusababisha kupata magonjwa zaidi kama ya moyo, Figo na Sukari" alifafanua Dkt. Myovela.

Aliongeza kuwa bado uhitaji wa wananchi wa kupata huduma za kibobezi na elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa maeneo ya vijijini ni mkubwa na kupitia kambi hiyo wamegundua kuwa wananchi hawana utamaduni wa kupima Afya zao hususani magonjwa yasiyo ya kuambukizwa.


Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Masasi Dkt. Abdul Rashidi ameshukuru ujio wa Madaktari kutoka BMH amesema watoa huduma wa Hospitali ya masasi wamejifunza na kupata uzoefu ambao wataendelea kuutumia kuwahudumia wananchi wa masasi.