Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa aanza kufanya tathimini ya kila Kurugenzi juu ya uboreshaji huduma za Matibabu na Changamoto za watumishi.
Na. Jeremiah Mbwambo, Dodoma 19/11/2025
Leo Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Makubi ameanza kutembelea ofisi za wakurugenzi wake ili kufanya majadiliano ya tathimini katika utekelezaji wa uboreshaji wa huduma kwa mteja, uendelezaji wa huduma, maagizo mbalimbali, changamoto za watumishi na kuwakumbusha wakurugenzi juu ya usimamizi wa watumishi wanaowaongoza katika kutumia weledi , maarifa na uchapa kazi wao kuboresha huduma za tuba na kusimamia majukumu yao .
"Tumezoea kuona wakurugenzi wakija kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji lakini leo natembelea ofisi zenu ili kufanya tathimini ya pamoja katika usimamizi wa maelekezo ya Viongozi, ubora wa huduma , ushirikishwaji wa taarifa za vikao na maelekezo yake" amesema Prof. Makubi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uuguzi Mwanaidi Makao ameeleza umuhimu wa kutembelewa na Mkurugenzi Mtendaji ili kufanya tathimini ya utekelezaji na kushuka chini kwa wasaidizi wake.
"Kwanza nikishukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuja kufanya tathimini kwa kuonana na kubwa kunitembelea ofisini kwangu hii imenifanya nione ninatakiwa kujiongeza zaidi katika kutekeleza majukumu yangu, pia imenipa uelewa mpana wa kuelewa namna ya kusimamia maelekezo yanayo tolewa"amesema Bi. Mwanaidi
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa ameanza vikao hivyo akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali, Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa ndani, kaimu mkuu wa kitengo cha uhakiki ubora wa huduma pamoja na kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma.