Mkurugenzi Mtendaji Prof Abel Makubi amekutana na Mheshimiwa Susan N. Namondo , Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Katika kuelekea hitimisho la maadhimisho ya Miaka 10 ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Mkurugenzi Mtendaji Prof Abel Makubi amekutana na Mheshimiwa Susan N. Namondo , Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na kujadiliana mambo mbali mbali ya Mashirikiano katika huduma za afya kwa kuhusisha pia wadau wa mashirika ya kimataifa. Katika maadhimisho yanayotegemea kufanyika tarehe 08 Mei 2026 , BMH pia itazindua mfuko maalumu wa kuwezesha huduma za Upandikizaji Uloto na Figo kwa Wananchi.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na mjumbe toka kwa Mwakilishi wa WHO na wajumbe wa Menejimenti ya BMH.
O9 Februari 2026, Dar es Salaam .