TUNAHITAJI MASHIRIKIANO NA TAASISI NYINGINE ILI KUTIMIZA DIRA YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA
Na. Jeremiah Mbwambo, 06/01/2026 Dodoma
Picha: Ludovick Kazoka
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi wakati akifungua kikao cha kutathimini hati zote za makubaliano ambazo Hospitali ya Benjamin Mkapa imeingia na Taasisi nyingine.
"Mimi ninaamini mashirikiano mazuri na Taasisi nyingine yanaweza kutufanikisha kufikia dira, peke yetu hatuwezi kufikia" amesema Prof. Makubi
Ameongeza kuwa ni muhimu kuwa wa wazi kabla au baada ya kuingia kwenye kusaini hati ya makubaliano
"Tunaposaini hati za makubaliano ni muhimu kutekeleza maana makubaliano yoyote yana pande mbili, ikiwa hayatekelezeki tuseme tusikae kimya" amesema Prof. Makubi
Tathimini hii ya hati za makubaliano ni hatua muhimu ya Hospitali ya Benjamin Mkapa kuimarisha huduma zake kupitia wadau wake.