Mwanzo / Huduma Zetu / Tunamshukuru mhe. rais wa tanzania kwa kutuletea matibabu.

Tunamshukuru mhe. rais wa tanzania kwa kutuletea matibabu.

Published on July 17, 2025

Article cover image

Hayo yamesemwa leo  na baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji katika magonjwa mbalimbali waliyo kuwa nayo

Mkazi wa Gitega Bw. Ntirampeba Clavert aliyekuwa na chuma mguuni amesema ujio wa madaktari wa Benjamin Mkapa umeokoa mguu wake 

"Nina mshukuru Rais wa Tanzania kwa kuwatuma madaktari kuja Burundi kututibu, mimi nilikuwa napata shida hata nilikuwa sijui nitatibiwaje madaktari hawa Mungu amewaleta kupitia Rais wa Tanzania" amesema Clavert.

Kwaupande wake Bw. Barashikiriye Jean mgonjwa aliye fanyiwa upasuaji ya kutibu tezi dume amesema nilikuwa nasikia maumivu makali 

"Ninawashukuru sana madaktari wa Benjamin Mkapa nilikuwa nasikia mwili unawaka moto lakini nimefanyiwa upasuaji sasa ninaendelea vizuri na maumivu siyasikii tena" amesema Bw. Jean 

Aidha Msaidizi wa Mkuu wa Hospitali ya Gitega Dkt. Arnaud Frank  amemshukuru Rais wa Tanzania kwa kuwaleta madaktari na Rais wa Burundi kwa kuwapokea madaktari 

"Binafsi ninawashukuru madaktari kwa kuwa na moyo wa kutufundisha kwani kunamatibabu yameletwa hapa sisi tulikuwa hatuyatoi lakini wagonjwa wamenufaika nasi madaktari tumeendelea kujifunza" alisema Frank

       WhatsApp Image 2025-07-17 at 10.27.04.jpeg