MMEJIUNGA NA FAMILIA YA BENJAMIN MKAPA ILI KUONGEZA TIJA, UBUNIFU NA KUBORESHA ZAIDI KIWANGO CHA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

Published: Mar 03, 2026
MMEJIUNGA NA FAMILIA YA BENJAMIN MKAPA ILI KUONGEZA TIJA, UBUNIFU NA KUBORESHA ZAIDI KIWANGO CHA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI cover image
Na. Jeremiah Mbwambo, Dodoma 24/02/2026
 
 
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Teophory Mbilinyi wakati akiwasilisha mada ya kujenga na kuimarisha mfumo fikra chanya kwa  watumishi wa Hospitali ya Beanjamin Mkapa.
 
 
 
"Familia ya Benjamin Mkapa imepiga hatua kubwa na imekuwa mfano wa kuigwa maana imeaminika na kupewa tuzo nyingi ikiwemo tuzo ya hospitali ya kwanza ya kanda kutoa huduma bora iliyo tolewa na Wizara ya Afya, hivyo mmejiunga nasi ili kuendeleza mafanikio ambayo tayari yamepatikana" amesema Bw. Mbilinyi.
 
 
 
Ameongeza kuwa mtumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa anatakiwa kuwa mleta suluhu kwenye matatizo
 
 
 
 "ili kufikia malengo ya kuendelea kuwa hospitali ya mfano katika kutoa huduma bora za afya  kwa wananchi, watumishi wa BMH lazima tuwe watoa suluhu ya matatizo badala ya kuwa walalamikaji” amesema Bw. Mbilinyi
 
 
 
Hospitali ya Benjamin imeandaa mafunzo kwa watumishi wapya na walio hamia ili kuwajengea uwezo wa kuendana na sheria na taratibu