Duka la Dawa
Hospitali ya Benjamin Mkapa inatoa huduma za dawa kwa wagonjwa ambao hawajafanya usajili wala kupita mapokezi, duka hili halimlazimishi mgonjwa mpaka apate matibabu kutoka kwa wataalamu wa afya wa Hospitali yetu. Duka hili linapatikana katika jengo la huduma za jamii ambalo liko karibu na jengo la pili la wodini au geti la kutokea.