Huduma za Maabara Maalum ya Moyo
Published on June 18, 2025

Maabara ya Catheterization (Cath Lab)
Hospitali ya Benjamin Mkapa
Maabara ya Catheterization (Cath Lab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa inatoa mazingira ya kisasa yanayowawezesha madaktari bingwa, wauguzi waliobobea na wataalamu wa teknolojia ya kitabibu kufanya taratibu maalum za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo na mfumo wa mishipa ya damu.
Taratibu hizi hufanywa kwa njia isiyo ya uvamizi mkubwa (minimally invasive), kwa kutumia catheter — mirija myembamba na laini inayopenyezwa kupitia mishipa ya damu hadi kwenye moyo au mishipa mikuu kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu au matibabu.
Taratibu na Magonjwa Yanayohudumiwa Katika Cath Lab
Hospitali ya Benjamin Mkapa ina uzoefu mkubwa katika kutambua na kutibu hali mbalimbali zifuatazo:
1. Magonjwa ya Mishipa ya Damu ya Moyo
- Kuziba au kujaa kwa mishipa ya moyo (Coronary Artery Disease)
- Angioplasty na Uwekaji wa Stent
Taratibu za kufungua mishipa iliyoziba kwa kutumia puto (baloon) na/au kuweka stenti ili kurudisha mtiririko wa kawaida wa damu.
2. Uchunguzi wa Mfumo wa Umeme wa Moyo
- Kutambua na kutibu arrhythmias (matatizo ya mpigo wa moyo) kupitia taratibu maalum za kielektroniki.
3. Upanuzi wa Valvu ya Moyo (Valvuloplasty)
- Kurekebisha au kupanua valvu za moyo zilizopungua au kuharibika ili kuboresha mtiririko wa damu.
4. Upimaji wa Moyo kwa Kutumia Katiheta (Cardiac Catheterization)
- Kupima shinikizo la damu, mtiririko wa damu, na utendaji wa vyumba vya moyo pamoja na mishipa mikuu ya damu.