Mwanzo / Huduma Zetu / Kliniki ya Pua,Koo na Masikio

Kliniki ya Pua,Koo na Masikio

Published on October 01, 2024

Service cover image

Utangulizi
Idara ya Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo (ENT) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ilianzishwa mwaka 2017 ikiwa na dhamira ya kutoa huduma bora na za kina kwa wagonjwa wenye matatizo ya masikio, pua na koo. Idara hii ilianza na daktari bingwa mmoja wa ENT, na imekua kwa kasi, ikiakisi dhamira yake ya kutoa huduma za hali ya juu kwa wagonjwa.


Huduma Zitolewazo
Idara ya ENT hutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa wa ndani na wa nje, zikiwemo:
Huduma za Ushauri na Uchunguzi: Kugundua na kutibu matatizo ya masikio, pua na koo kama vile upotevu wa kusikia, sinusitis, na matatizo ya koo.
Upasuaji: Kufanya upasuaji wa kawaida na wa dharura kwenye maeneo ya masikio (otology), pua (rhinology), na koo, ikiwemo upasuaji wa sinus, kuondoa tonsils (tonsillectomy), na adenoids (adenoidectomy).
Kitengo cha Audiolojia: Hutoa huduma za uchunguzi wa kusikia na vifaa vya kusaidia kusikia kwa ajili ya kuboresha afya ya usikivu.
Kitengo cha Tiba ya Matatizo ya Hotuba: Huwasaidia wateja wenye changamoto za mawasiliano na hotuba.
Huduma za Uchunguzi: Kutumia vifaa vya kisasa kama audiometri, tympanometri na picha (imaging) kwa uchunguzi wa kina.
Huduma za Kinga: Kutoa elimu ya afya na kufanya kampeni kwa jamii kuhusu afya ya ENT ili kuongeza uelewa.
Timu Shirikishi (MDT): Idara inashirikiana na fani nyingine katika kutoa huduma kwa wagonjwa na pia kushiriki katika timu shirikishi za kitabibu kwa magonjwa mbalimbali.
Ushirikiano: Idara inashirikiana na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, zikiwemo taasisi za elimu kama Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mafunzo na Huduma za Outreach: Idara ni kituo cha mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari kutoka UDOM na wanafunzi wa elective kutoka taasisi mbalimbali. Pia hutoa huduma za outreach kwa jamii kupitia programu maalum za hospitali.


Rasilimali Watu
Idara ya ENT ina timu yenye utaalamu na uzoefu mkubwa ikijumuisha:
Madaktari Bingwa wa ENT: Wataalamu watano, wakiwemo wawili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wataalamu wa Usikivu na Tiba ya Hotuba: Wakitoa huduma maalum katika maeneo yao ya utaalamu.
Wafanyakazi Wasaidizi: Wauguzi, mafundi na wataalamu wengine wanaoshirikiana kuhakikisha huduma shirikishi na bora kwa wagonjwa.


Mikakati ya Baadaye
Idara ya ENT imejipanga kupanua huduma na miundombinu yake kwa kujumuisha:
Jengo Maalum la ENT: Mpango wa kujenga jengo la kisasa litakalowezesha utoaji wa huduma maalum na upasuaji mgumu wa pua, masikio na koo.
Huduma za Kibingwa Zaidi: Kwa kushirikiana na washirika wa kimataifa na hospitali nyingine nchini ili kutoa huduma maalum kama upasuaji wa kutumia endoscope na huduma za saratani ya njia ya hewa na chakula (aerodigestive cancers).
Kituo cha Umahiri (Center of Excellence): Kuanzisha kituo cha kikanda kwa huduma za ENT, utafiti na mafunzo.
Kuongeza Huduma kwa Jamii: Kupanua kampeni za uchunguzi na elimu ya afya kwa jamii, hasa katika maeneo yasiyofikika kirahisi.
Mafunzo Endelevu kwa Wafanyakazi: Kuhakikisha timu inaendelea kuwa na ujuzi wa kisasa na dhamira ya kutoa huduma bora za ENT.