Mfumo wa Chakula
Published on June 30, 2025

Wasifu wa Kitengo cha Magonjwa ya Mfumo wa Chakula (Gastroenterology) – Hospitali ya Benjamin Mkapa
1. Sifa Muhimu (Faida ya Ushindani)
Upatikanaji na Huduma Jumuishi:
Kitengo cha Gastroenterology kinatoa huduma maalum kwa magonjwa ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kupitia kliniki za ratiba na huduma za dharura. Huduma hutolewa kwa haraka kwa kutumia vifaa vya kisasa vya upimaji wa ndani ya tumbo (endoscopy).
- Tuna vifaa vya kisasa vya Upper GI na Lower GI endoscopy
- Huduma jumuishi na maabara, famasia na mionzi kwa uchunguzi na matibabu kamili
2. Huduma Zitolewazo
• Utambuzi na matibabu ya magonjwa ya mfumo wa chakula
• Upper GI endoscopy (esophagogastroduodenoscopy)
• Lower GI endoscopy (colonoscopy na sigmoidoscopy)
• Matibabu ya magonjwa ya ini na kongosho
• Matibabu ya vidonda vya tumbo na gastritis
• Matibabu ya Inflammatory Bowel Disease (IBD)
• Upimaji na matibabu ya homa ya ini (hepatitis)
• Ushauri wa kitaalamu kwa wagonjwa waliolazwa
3. Timu ya Watoa Huduma
• Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Tumbo (Gastroenterologists)
• Madaktari wa mafunzo ya kitaalam (Registrars)
• Wauguzi wa Endoscopy
• Wauguzi wa kawaida waliobobea
• Wataalamu wa lishe (Nutritionists)
• Wanasayansi wa Maabara
4. Idadi ya Wagonjwa kwa Mwaka
Tunahudumia wastani wa wagonjwa 4,500 kwa mwaka, wakiwemo wanaofanyiwa endoscopy na wanaohudumiwa kliniki.
5. Jinsi ya Kupata Huduma Zetu
- Huduma za Endoscopy zinapatikana kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2:00 asubuhi hadi 3:30 jioni
- Kliniki ya Gastroenterology hufanyika kila Alhamisi saa 2:00 asubuhi hadi 3:30 jioni
- Huduma za ushauri kwa wagonjwa waliolazwa zinapatikana saa 24 kila siku
- Kwa ajili ya miadi, rufaa, au huduma za endoscopy, tafadhali wasiliana moja kwa moja na kitengo chetu (kwa sasa hatuna namba ya simu ya miadi)
6. Ushirikiano wa Kitaasisi
- Ushirikiano wa karibu na Maabara na Idara ya Mionzi kwa ajili ya uchunguzi wa hali ya juu na vipimo vinavyohusiana na mfumo wa chakula
7. Mpango wa Kuboresha Ubora wa Huduma
- Mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalamu wetu kuhusu mbinu mpya za endoscopy na dharura za magonjwa ya mfumo wa chakula
- Tathmini za mara kwa mara za huduma kwa wagonjwa ili kuboresha njia za utoaji huduma
- Elimu kwa wagonjwa kuhusu afya ya mfumo wa chakula na ushauri wa lishe
8. Maendeleo ya Hivi Karibuni
- Kupanua huduma za endoscopy ya matibabu ikijumuisha sclerotherapy
- Kuimarisha upimaji wa hepatitis na huduma kwa wagonjwa wenye magonjwa ya ini
Taarifa za Mawasiliano
📞 Kwa miadi na maulizo:
Kwa sasa hatuna namba maalum ya simu kwa ajili ya miadi – tafadhali tembelea hospitali au wasiliana kupitia ofisi kuu kwa masailiano yapatikanayo katika tovuti.