Mwanzo / Huduma Zetu / Huduma ya Upandikizaji wa Figo

Huduma ya Upandikizaji wa Figo

Published on June 18, 2025

Service cover image

 Upandikizaji wa Figo

Upandikizaji wa figo ni njia bora na inayopendekezwa zaidi ya tiba mbadala ya figo kwa wagonjwa waliopata kushindwa kabisa kwa figo. Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imejikita katika kuwarejeshea matumaini mapya wagonjwa wote walioko katika hatua ya mwisho ya kushindwa kwa figo, kwa kuwasaidia kurejea kwenye maisha bila kutegemea mashine za kusafisha damu (dialysis). Tangu mwaka 2018 ambapo upandikizaji wa kwanza wa figo ulifanyika kwa mafanikio kwa wanandoa wa kwanza, BMH imefanya zaidi ya upandikizaji wa figo 50.

Hospitali, kwa kushirikiana na Tokushikai Medical Group kutoka Japan na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ilianza kutoa huduma za upandikizaji wa figo mwaka mmoja baada ya upandikizaji wa kwanza kufanyika nchini Tanzania mwaka 2017. Baada ya mkakati uliopangwa kwa umakini, timu ya wataalamu kutoka BMH walipata mafunzo maalum nchini Japan. Hospitali ilionesha dhamira yake ya kuboresha huduma ya figo kwa kuanzisha huduma hii ya upasuaji inayobadili maisha, ambayo kwa mara ya kwanza duniani ilifanyika mwaka 1954.

BMH inatoa huduma ya Upandikizaji wa Figo kutoka kwa Mtoa Hai wa Figo (Living Donor). Timu yetu ya madaktari bingwa wa upandikizaji, madaktari wa figo (nephrologists), wauguzi, wataalamu wa kazi za kijamii na wataalamu wa lishe imejikita kutoa huduma yenye huruma, inayomlenga mgonjwa na kuratibiwa vyema tangu hatua ya awali ya tathmini ya upasuaji, wakati wa upasuaji hadi ufuatiliaji wa baada ya upasuaji.

Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, BMH inalenga kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji wa Figo, chenye mkazo katika kufanya tafiti za kisasa na kutoa mafunzo, ili kuboresha upatikanaji wa huduma za upandikizaji na afya ya figo kwa ujumla. Ushirikiano wetu wa karibu unatuwezesha kutoa huduma bora za kisasa katika nyanja zote za mfumo wa upandikizaji.

Kwa huduma au maulizo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia: +255 (0) 735 000 002.

                                                                          figoo.jpg