Huduma ya Magonjwa na Afya ya Akili
Published on June 08, 2025

Huduma za Kibingwa za Afya ya Akili katika Hospitali ya Benjamin Mkapa zilianza mwaka 2018 kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Lengo likiwa kutoa huduma bora za kibingwa za king ana matibabu ya magojwa ya akili, huduma za utengamao kwa watu walioathirika na magonjwa ya akili, mafunzo na utafiti kwa kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa na kwa kutumia madaktari bingwa na wabobezi, ubunifu na kutumia vifaa tiba vya teknolojia ya kisasa. Huduma za afya ya akili zinahitajikwa kwa kila mtu hivyo, zinatolewa kwa kushirikisha na kushirikiana na huduma nyinigine hospitalini.
· Huduma za Kibingwa za Afya ya akili kwa BMH zimegawanyika katika maeneo yafuatazo;
· Huduma za magonjwa ya akili yanayojidhihirisha kama magonjwa mengine ya mwili: Consultation-Liason (Psychosomatic) Psychiatry
· Huduma za magonjwa ya akili kwa watoto na vijana: Child and Adolescent Psychiatry
· Huduma za magonjwa ya akili yanayohusiana na mishipa ya fahamu/neurolojia: Neuropsychiatry
· Huduma kwa watu walioathirika na pombe na dawa za kulevya: Addiction Psychiatry
· Huduma za utengamao kwa watu walioathirika na magonjwa ya akili: Rehabilitation Psychiatry
· Huduma za elimu na kinga ya magonjwa ya akili kwa jamii: Community Psychiatry
Aina za Huduma:
Aina za Huduma za Afya ya Akili zinazotolewa katika Hospitali ya BMH ni hizi zifuatavyo:
1) Ushauri na Uchunguzi
ü Uchunguzi wa ki-saikolojia (psychometric investigation)
ü Uchunguzi wa ki-maabara (laboratory investigation), ikiwemo; Urine Toxicology
ü Uchunguzi wa ki-radiolojia (radiological imaging), ikiwemo; Video EEG
2) Matibabu ya Dawa (Psychopharmacology) na Matibabu Maalumu,
ü Ikiwemo “Medication Assisted Treatment” na “Detoxification” kwa wenye Uraibu
ü Electroconvulsive Therapy (ECT) na Deep Brain Stimulation (DBS) kwa watu wenye magonjwa ya akili yaliyoshindikana kwa tiba ya dawa
3) Matibabu ya Ushauri Nasihi wa Kibingwa (Psychotherapy)
ü Kwa mtu mmoja (Individual Counseling)
ü Kwa familia na wenza (Family/Couple Counseling)
4) Matibabu ya Utengemao
ü Tiba kwa njia ya Kazi (Occupational Therapy)
ü Huduma Maalumu za Utengemao (Rehabilitation services)
· Usikivu na Uongeaji (Speech and Audiology therapy)
· Mazoezi Tiba (Physiotherapy)
Utaratibu wa Utoaji Huduma BMH:
a) Huduma za Nje (Outpatient Services)
ü Kliniki za Kawaida (Siku ya Jumatatu na Jumatano)
ü Kliniki ya “Executive” (Kila Siku ya Juma/Mwisho wa Juma)
ü Kliniki ya “Fast Track/Royal” (Kila Siku ya Juma/Mwisho wa Juma)
b) Huduma za ulazwa (Inpatient Services)
ü Kila Siku
c) Huduma za Mafunzo na Elimu kwa Jamii: kwa utaratibu maalum
Usimamizi na Uendeshwaji wa Huduma:
Huduma zipo chini ya Kurugenzi ya Tiba na zinasimamiwa na;
ü Dkt. Isack C. Rugemalila
Daktari Bingwa wa Afya ya Akili na Matibabu ya Uraibu (BMH)
ü Prof. Azan Nyundo
Daktari Bingwa wa Afya ya Akili (UDOM)