Mwanzo / Kurasa / Huduma za Haraka

Huduma za Haraka

Published on November 13, 2024

Article cover image

 

KLINIKI YA "FAST TRACK"

Kliniki ya Fast Track ipo ghorofa ya pili ya jengo la awamu ya kwanza. Kliniki hii imeundwa kutoa huduma za afya kwa haraka, kwa uhakika na kwa ubora wa hali ya juu kwa wateja wanaoihudhuria.

Kliniki ipo chini ya uongozi wa Dkt. SAGUDA na Sr. NDOSI, na inafanya kazi siku zote za wiki kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri siku za kazi (Jumatatu hadi Ijumaa), na kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana siku za mwisho wa wiki (Jumamosi na Jumapili).

Madaktari, wauguzi na wataalamu wengine waliobobea na wenye uzoefu mkubwa watakuwa wanahudumia mgonjwa mmoja kwa wakati mmoja wakizingatia mahitaji binafsi ya kila mmoja.

Kliniki imewekwa vifaa vya kisasa, mfumo wa kielektroniki wa kurekodi taarifa za wagonjwa, na imeundwa mahsusi kuunga mkono wagonjwa pamoja na familia zao. Kliniki ina vyumba vinne vya ushauri (Consultation rooms), chumba kimoja cha uangalizi (Observation), sehemu ya mapumziko (Lounge), Maabara ya kuchukua sampuli (Phlebotomy), Duka la Dawa (Pharmacy) na chumba cha Ultrasound. Sehemu ya kungojea ina runinga kubwa inayotoa elimu ya afya kila siku kuhusu masuala mbalimbali.

Tumejizatiti kutoa huduma salama zaidi, bora zaidi na yenye kuridhisha kwa kiwango cha juu, huku tukihakikisha unapata nafuu kwa haraka.

 

Taarifa Muhimu:

  1. Wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa siku hiyo hiyo (Day Surgery), vipimo vya moyo (Cardiac Evaluation) au kulazwa, watasindikizwa na kuhudumiwa kulingana na mpangilio wa huduma wa vitengo husika.
  2. Wagonjwa walioko kwenye foleni watashauriwa wakae kwenye sehemu ya kungojea wakisubiri huduma inayofuata.
  3. Wagonjwa wote watapewa vipeperushi vyenye mwongozo wa huduma na maelezo ya nini cha kutarajia.
  4. Kwa maswali, maoni au nafasi ya miadi, tafadhali piga simu 0734331099 au tutumie barua pepe kupitia info@bmh.or.tz
  5. Kwa lengo la kuboresha huduma zetu na kuhakikisha ubora unaendelea kuimarika, wagonjwa wataombwa kujaza dodoso fupi kutoa maoni yao kuhusu huduma waliyopewa. Ushiriki ni wa hiari na unathaminiwa sana.

 

Tunawatakia uzoefu bora na uponaji wa haraka. Faragha yako, usalama na afya yako ni kipaumbele chetu. Tuna utaalamu na uzoefu unaohitajika kukupa wewe na familia yako huduma bora, ya kisasa na inayotegemea ushahidi wa kitaalamu na teknolojia ya kisasa kabisa.

Kwa miadi au maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia +255 (0) 735000002